Usajili

MZAMIRU ATOA KAULI TATA KUHUSU YANGA KUMSAJILI, MANARA AFUNGUKA

Wakati sakata la kiungo wa Simba Mzamiru Yassin akihusishwa kuhusu kuihama timu hiyo na kutua Yanga, mchezaji huyo amesababisha gumzo lingine kuhusu usajili wake.

Taarifa hizo zimekuja wakati huu ambapo kuna dirisha dogo la usajili linaendelea tangu lilipofunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

Kutumia ukurasa wake wa Instagram, kiungo huo aliandika ujumbe huu:

“Wakati unapofanya maamuzi kwa wakati maalumu huna budi kumshukuru mwenyeziMungu kwani bila yeye wewe si kitu, waachie walimwengu waendelee kuongea midomo mali yao.”

Mara baada ya ujumbe huo ikaonekana kama maamuzi anayoyazungumzia ni kuelekea Yanga, lakini alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema hajui chochote kuhusu suala hilo kwa kuwa Mzamiru bado ni mchezaji wa Simba.