Usajili

SIMON MSUVA MPAKA RAHA, ATUPIA TENA, TIMU YAKE YASHINDA MABAO 4-1

Mshambuliaji Simon Msuva, ameendelea kuwa na maendeleo mazuri katika kikosi cha Difaa Hassan El - Jadida baada ya kufunga bao moja na kuchangia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Khouribga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco ulifanyika kwenye Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan.

Msuva ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga ya Tanzania alifunga bao lake katika dakika ya 71, likiwa la nne katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola.

Mabao mengine matatu ya DHJ yote yalifungwa na mshambuliaji chipukizi Mmorocco, Hamid El Ahadad dakika za 30, 40 na 57.

Kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida inafikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 19 za mechi 10.