Usajili

VIDEO: ALLY MAYAY APONGEZA SIMBA KUMUUZIA HISA MO DEWJI

Siku chache tangu Klabu ya Simba itangaze kupitia mabadiliko ya mfumo wa uongoziaji wa klabu hiyo, ambapo sasa kutakuwa na mfumo wa hisa huku mwanachama wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'Mo'

akikabidhiwa majukumu ya kumiliki sehemu ya hisa, kumekuwa na maoni mengi kuhusu uamuzi huo.

Awali ulionekana kuwa utakuwa uamuzi mgumu kwa kuwa ni kitu kigenbi katika soka la Tanzania, mchakato kama huo pia ulikuwa ukifanywa na Yanga lakini bado hawajafikia kwenye hitimisho kama ilivyo kwa Simba.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele ameipongeza hatua iliyochukuliwa na Simba kufuatia kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, bonyeza video kutazama video kamili ya kile alichokizungumza.