Usajili

Kocha Mkuu wa Singida United, Fred Felix Minziro, amekubali bila kinyongo kuyaacha majukumu hayo chini ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm huku akisema kuwa ujio wa kocha huyo utasaidia kutoa dozi kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.