Usajili

MSHAMBULIAJI Wa Majimaji FC, ya Songea, Marcel Boniventure 'Kaheza', amewabwaga Emmanuel Okwi pamoja na John Bocco, katika kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwezi April kunako Ligi kuu Tanzania Bara (VPL).

KIUNGO mkabaji wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ufaransa, N`golo Kante, amesema kuwa hayupo tayari kuondoka Chelsea na kuelekea sehemu nyingine hata kama Chelsea haitafuzu kucheza michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya (UEFA).