Wachezaji

Vincent Bossou

Vincent Bossou
Defender

 • Full Name

  Vincent Bossou

 • Date of Birth

  February 7th, 1986

 • Place of Birth

  Togo

 • Height

  6′ 4″

 • Weight

  75kg

Career

 • Matches: 96
 • Goals: 22
 • Discipline: 01
 • Passing: 3 fouls against
 • Club Name: Young Africans Sports Club
 • Club Debut: June 9th, 2015
Young Africans Sports Club 96 Matches Played

Overview

Beki wa kati wa Young Africans Sports Club ‘Yanga’ ambaye alizaliwa
Februari 7, 1986, eneo la Kara, Togo. Ni mmoja wa wachezaji warefu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Bossou ni raia wa Togo ambaye urefu wake ni futi 6 na inchi 3, akiwa Yanga amekuwa akivaa jezi namba 9.

Alianza kucheza soka mwaka 1997  katika timu ya vijana ya Maranatha F.C ya Togo, baadaye alipokua akahamishiwa kwenye timu ya wakubwa ya Maranatha F.C. ambapo alidumu hapo kuanzia mwaka 2006 hadi 2009.

Mwaka 2010 alisajiliwa na Étoile Sportive du Sahel na kupewa mkataba wa miaka miwili lakini miezi mitatu tu ilitosha yeye kuwepo hapoa, mkataba wake ukavunjwa na baadaye akarejea kwenye timu ya
Maranatha F.C mwaka huohuo wa 2010.

Aliamua kuhamia kwa muda Vietnam kuendelea kucheza soka, mwaka 2011 hadi 2012 alikuwa ni mchezaji wa Navibank Sài Gòn, kisha mwaka 2013 akahamia Becamex Bình Dương, ambapo hakudumu muda mrefu akahamia TDC Bình Dương mwaka huohuo wa 2013.

Mwaka 2014 akasajiliwa na An Giang, mwaka mmoja baadaye yaani 2015 akatua Goyang Hi FC, kisha mwaka 2015 akahamia Yanga ambapo ndipo alipo hadi sasa.

Amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Togo kuanzia mwaka 2007 hadi sasa, alikuwemo katika kikosi cha Togo kilichoshiriki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.