Wachezaji

Simon Msuva

Simon Msuva
Forward

 • Full Name

  Simon Msuva

 • Place of Birth

  Tanzania

 • Height

  165 cm

 • Weight

  68kg

Career

 • Matches: 85
 • Goals: 30
 • Discipline: 3 fouls against
 • Passing: 23
 • Club Name:
85 Matches Played

Overview


Simon Msuva ambaye amesajiliwa na  Difaa El Jadida ya Morocco kwa msimu wa 2017 , alikua akitumika Kama winga na mshambuliaji katika timu ya Yanga. 


Msuva alizaliwa Oktoba 2, 1993 jijini Dar es Salaam pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na ile ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’

Msuva amewahi kuichezea Azam FC mwaka 2010 hadi 2011, Moro United (2011-2013) kabla ya kutua Yanga mwaka 2013 ambapo ndipo alipo hadi sasa.

Mataji na tuzo ambazo amefanikiwa kupata ni: Mfungaji Bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (2014-2015 – alifunga mabao 17), Mfungaji Bora Kombe la Mapinduzi 2015 (mabao matano). Mfungaji Bora Uhai Cup 2010.

Kitu kingine ni kuwa kutokana na staili yake ya kufunga kisha anashangilia, inatokana na kuwa aliwahi kuwa dansa katika kituo cha Tanzania House of Talent (THT) kati ya mwaka 2004 hadi 2005.

ALIKOTOKA
Kutokana na kuwa vipaji viwili na vyote akiamini kuvimudu vilivyo, 2006 Msuva alijiunga na timu ya mchangani inayojihusisha na ukuzaji wa vipaji vya vijana wadogo ijulikanayo kwa jina la ‘Wakati Ujao’.

Akicheza kama mshambuliaji wa kati na wakati mwingine winga,  Msuva alijiunga na timu ya kukuza vipaji vya vijana ya Azam 2008 ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa.

AVUNJIKA
Ndoto zake za kucheza soka nusura zifikie ukingoni baada ya kuvunjika mguu mwishoni mwa mwaka 2008, lakini akang’ara katika michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola 2009 na 2010 iliyompa fursa ya kuitwa katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’.

ATUA MORO UTD
Kung’ara kwake katika kikosi cha Serengeti Boys nchini Sudan, kulitiwa Moro United, waliomsajili katika kikosi chao cha vijana 2010 ambako alifanya kweli na kuibuka mfungaji bora wa michuano ya vijana wa timu za Ligi Kuu ya Bara maarufu kama Uhai Cup kisha kupandisha hadi kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya Morogoro.

Baba yake, Mzee Hapygod Msuva, alieleza jijini hapa hivi karibuni kuwa mtoto wake huyo alisajiliwa kwa Sh. 250,000 kujiunga na Mro United akitokea kituo cha Azam FC.

ARUDI CHAMAZI
Mwaka 2011, alihama Moro United na kurejea Azam FC ambako alipelekwa kikosi B na hakupewa nafasi kubwa katika kikosi cha kwanza, jambo ambalo liliushawishi ubongo wake kurejea Moro United 2012 na Yanga wakamnasa.

SHABIKI WA RONALDO, DOMAYO
Msuva ni shabiki mkubwa wa mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo na kiungo wa Azam FC, Frank Domayo. Anasema anampenda Ronaldo, kutokana na aina ya uchezaji wake, lakini Domayo ni zaidi ya mchezaji na rafiki kwake.

Msuva ambaye kwa sasa ni kiongozi wa Yanga katika kushangilia mabao, pia ni shabiki wa Manchester United ya England.

ELIMU YA DARASANI
Mkali huyo wa mabao alizaliwa Oktoba 2, 1993 na kusoma Shule ya Msingi ya Lions iliyopo Magomeni, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

AWANIWA NA SIMBA
Mwishoni mwa mwaka jana, uongozi wa Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope, ulituma maombi ambayo hayakuwa rasmi kwa uongozi wa Yanga ukitaka kumsajili Msuva.

Jambo hilo lilionekana kuwakera baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakitaka kumdunda nyota huyo kwa madai ya kucheza kinazi dhidi ya Simba katika mechi wanazofungwa na watani wao hao wa jadi.