Wachezaji

Mbaraka Yusuph

Mbaraka Yusuph
Forward

 • Full Name

  Mbaraka Yusuph

 • Place of Birth

  Dar es Salaam

 • Height

  Futi 5

 • Weight

  68kg

Career

 • Matches: 20
 • Goals: 11
 • Club Name: Kagera Sugar
 • Previous Club: Simba Sports Club
Kagera Sugar 20 Matches Played

Overview

Mbaraka Yusuph ni mshambuliaji wa Kagera Sugar na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Msimu wa 2016/17 ni msimu wake wa pili kucheza katika Ligi Kuu Tanzania Bara, alianza kucheza katika msimuwa 2015/16 katika timu hiyohiyo ya Kagera Sugar ambapo alifanikiwa kufunga mabao 8 katika msimu wake wa kwanza tu.

ALIPOTOKEA
Mbaraka ni zao kutoka Klabu ya Simba kabla, ni mmoja wa wachezaji waliocheza katika kikosi cha Simba B walio unda timu kali ya vijana akiwa na kina Ramadhani Singano, Abdallah Seseme, Wiliam Lucian,  Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Isihaka Rajab na wengine chini ya mwalimu Matola na walifanikiwa kunyakua ubingwa wa Banc ABC kwa kumfunga Mtibwa goli 4 kwa mbili

Licha ya kuwa na mwanzo mzuri kwenye timu ya vijana ya Mnyama, Mbaraka Yusuph akufanikiwa kupenya kwenye timu ya kikosi cha kwanza cha Wekundu wa Msimbazi

SIMBA WAMTAKA TENA
Baada ya mambo kumuendea kombo na kushindwa kulishawishi benchi la ufundi la kikosi cha kwanza, Simba iliamua kumtoa straika huyu kwa mkopo kwenye timu ya Kagera Sugar, msimu wa kwanza tu ndani ya Kagera alifanya vizuri kwa kufunga magoli zaidi ya 7 na kufanya Simba kutaka kumrudisha tena baada ya kiwango kizuri kipindi cha mkopo

AINGIA MGOGORO NA SIMBA
Baada ya kufanya vizuri Kagera ndipo Simba walivutiwa kumrudisha kundini lakini kinda huyu aligoma kurudi akidai kuwa hana mkataba na Mnyama huku Simba wao wakidai kuwa Yusuph amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake

Mgogoro huu kati ya Simba na mchezaji huyu uliamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mbaraka kushinda kesi hiyo yeye hautambui.

“Sina mkataba wowote na Simba, mkataba uliopo sikusaini mimi alisaini Patrick, mwaka huu walitaka kuniongeza mkataba wa miaka mitatu lakini ilishindikana kwa sababu pesa waliyotaka kunipa ilikuwa ni ndogo, ningesaini ingekuwa miaka minne, nilichokifanya nilichukuwa mkataba huo ili nikausome ambapo sijaurudisha mpaka sasa.

“Wameniwekea pingamizi kwamba ni mchezaji wao, hata kama TFF watasema nirudi Simba sitaweza kurudi tena hapo ni bora nikae tu pasipo kucheza maana wanachonifanyia si sahihi, kabla nilitaka kukubali kumalizia huo mwaka mmoja kwa kutumia busara tu ila baadaye niliona sitendewi haki ndiyo maana nilienda kusaini Kagera Sugar mkataba wa mwaka mmoja,” aliwahi kunukuliwa Mbaraka akisema.

MIPANGO YAKE
Anasema malengo yake ni kufuata nyayo za mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye anakipa Ubelgiji kwenye klabu ya KRC Genk

APATA TUZO
Aprili 4, 2017, TFF ilimtangaza kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.

Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.

Katika mwezi huo ilichezwa raundi moja tu na Mbaraka ambaye alicheza kwa dakika zote 90 aliisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu zilizoifanya timu yake kubaki katika nafasi ya nne (4) katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo.

Katika mchezo huo mmoja, Mshambuliaji huyo alifunga goli moja, na alionyesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la kadi.

Kwa kushinda tuzo hiyo, Mbaraka atazawadiwa kitita cha Sh 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC.