Wachezaji

Mrisho Ngassa

Mrisho Ngassa
Forward

 • Full Name

  Mrisho Khalfan Ngassa

 • Date of Birth

  April 12th, 1989

 • Place of Birth

  Mwanza

 • Height

  175 cm

 • Weight

  68 kg

Career

 • Matches: 87
 • Goals: 8
 • Discipline: 3 fouls against
 • Passing: 23
 • Club Name: Mbeya City Council Football Club
 • Club Debut: March 24th, 2009
 • Previous Club: Kagera Sugar
Mbeya City Council Football Club 87 Matches Played

Overview

Mrisho Khalfani Ngasa alizaliwa Aprili 12, 1989, ni mchezaji wa Kitanzania ambaye amecheza soka kwa muda mrefu katika klabu tofauti, za ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania.

Kwa sasa ni mchezaji wa Mbeya City ya Mbeya ambayo inashiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara maarufu kwa jina la Ligi Kuu ya Vodacom.

Mrisho Ngassa ni mtoto wa Khalfani Ngassa ambaye ni kiungo mshambuliaji wa zamani wa Pamba, Simba na Taifa Stars ambaye kwa sasa makazi yake yapo Mwanza, Tanzania.

Ngassa alizaliwa Mwanza na kukulia katika mji huo ulipo Kanda ya Ziwa, na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kirumba, mitaa ambayo ndipo alipokulia.

Mrisho Ngassa hakupata elimu kubwa kwa kuwa kipaji chake cha soka kilimfanya akaongeza bidii kwenye kucheza soka badala ya kusoma. Wakati anakua kisoka alikua pamoja na vijana wengi ambao baadaye walikuja kucheza katika timu kubwa wakiwemo Jerry Tegete, Henry Joseph na Kelvin Yondani.

ATUA YANGA
Alijiunga Yanga mwishoni mwa mwaka 2006 akitokea Kagera Sugar ya Kagera, ambapo chini ya utawala wa makocha tofauti alionyesha uwezo mkubwa na kuendelea kuwa chaguo la kwanza, kiasi kwamba akawa kipenzi cha mashabiki na viongozi wa Yanga.

Baadhi ya makocha waliomfundisha Ngassa akiwa Yanga ni Jack Chamangwana, Sredojevic Milutin 'Micho', Razak Siwa, Dusan Kondic na Maximo

MAJARIBIO WEST HAM UNITED
Aprili 2009, Ngassa alialikwa kufanya majaribio katika kikosi cha West Ham United kinachoshiriki kwenye Ligi Kuu ya England ‘Premier League’. Hakufanikiwa katika majaribio hayo na kurejea Tanzania.

KUJIUNGA AZAM FC
Mei 21, 2010, Ngassa aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa zaidi ndani ya Tanzani baada ya kujiunga na Azam FC akitokea Yanga kwa kiasi cha fedha ambacho ilidaiwa kuwa ni shilingi milioni 98.

MAJARIBIO MAREKANI
Julai 2011, Ngassa alienda kufanya majaribio ya kucheza soka la kuliowa katika timu ya Seattle Sounders FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Marekani (Major League Soccer), alipata nafasi ya kucheza katika mechi ya kirafiki ya timu hiyo dhidi ya Manchester United ambapo aliingia kipindi cha pili akirokea benchi. Hakufanikiwa katika majaribio hayo akarejea Tanzania.

AJIUNGA SIMBA
Agosti 2012, Ngassa alijiunga na Simba, timu ambayo ni wapinzani wakubwa wa Yanga. Alisajiliwa na Simba kwa mkopo akitokea Azam FC ambapo alishindwana na uongozi wa klabu hiyo.

Baada ya kumalizika kwa msimu wa 2012/13, mkataba wake ukawa umemalizika, Ngassa alirejea kwenye klabu yake ya zamani ya Yanga.

Baada ya kuitumikia Yanga kwa miaka miwili, Mrisho Ngassa aliondoka kwenda kucheza soka South Africa katika Klabu ya Free State Stars ambapo alisaini mkataba wa miaka minne, hiyo ilikuwa mwaka 2015.

Hakudumu muda mrefu, mwaka 2016 alivunja mkataba na kurejea Tanzania kisha baada ya muda akaenda kucheza soka Uarabuni, akajiunga katika timu ya Fanja ya Oman.

Fanja nako hakudumu muda mrefu, mwaka 2017 akarejea Tanzania akidai amerejea kwa ajili ya matibabu ya goti lililokuwa likimsubua, lakini wiki kadhaa baadaye akatangaza kujiunga na Mbeya City ambapo ndipo alipo hadi sasa, ikidaiwa amesaini mkataba wa muda mfupi.

TIMU YA TAIFA
Baada ya kutoa mchango mkubwa katika ngazi ya klabu, pia aliweza kufanikiwa katika ngazi ya timu za taifa ambapo alikuwa tegemeo la kwanza katika kikosi cha kocha wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo na makocha wengine waliofuata, pia aling’ara katika kikosi cha taofa cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’.

Ngassa alivaa jezi ya Taifa Stars kwa mara ya kwanza Machi 29, 2008 mjini Nairobi wakati wa mchezo wa raundi ya kwanza wa harakati za kuelekea katika fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani zitakazofanyika Ivory Cost ambazo mwishowe Taifa Stars ilifanikiwa kufuzu.

Katika mchezo huo Ngasa aliingia kwenye Uwanja wa Nyayo katika dakika 65 na tangu wakati huo aliendelea kuwa tegemeo.


MATAJI
Yanga
Tanzanian Premier League: 2007–08, 2008–09,2009-1O,2010–11,2011–12,2012–13,2013–14

Tusker Cup: 2007, 2009

Azam FC
Kagame Interclub Cup: Runner-up 2012

Tuzo binafsi
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu: 2009–10[10]
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu: 2010–11
Mfungaji Bora wa Cecafa Cup: 2009
Mfungaji Bora Ligi ya Mabingwa Afrika: 2013–1014 (alifunga mabao 6 katika mechi nne)
Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu Tanzania 2014/2015: Aprili