Wachezaji

Mwinyi Kazimoto

Mwinyi Kazimoto
Midfielder

 • Full Name

  Mwinyi Kazimoto

 • Date of Birth

  December 25th, 1988

 • Place of Birth

  Mwanza

 • Height

  158 cm

 • Weight

  65 kg

Career

 • Matches: 65
 • Goals: 18
 • Discipline: 3 fouls against
 • Passing: 23
 • Club Name: Simba Sports Club
 • Club Debut: July 10th, 2007
 • Previous Club: JKT Ruvu Stars
Simba Sports Club 65 Matches Played

Overview

Kiungo wa Simba ambaye rekodi zinaonyesha alizaliwa Desemba 25, 1988, ni mmoja wa wachezaji wazoefu katika timu hiyo ambapo amecheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda mrefu, pia amewahi kucheza soka nje ya nchi.

Rekodi za kuanza kucheza timu kubwa zinaonyesha alianza kucheza mwaka 2007 katika timu ya JKT Ruvu Stars ambayo inamilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), alidumu hapo hadi mwaka 2011.

Mwaka 2011 alisajiliwa na Simba ambapo alianza taratibu lakini baadaye alishika kasi na kuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza ambapo alicheza mechi nyingi kubwa.

Mwaka 2013, Klabu ya Simba ilifanikiwa kumuuza Uarabuni katika timu ya Al Markhiya ambapo alicheza huko kwa miaka miwili.

Mwaka 2015 alirejea Simba na yupo hadi sasa. Katika vipindi kadhaa ameichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na ile ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars tangu mwaka 2009.