Wachezaji

Haruna Niyonzima

Haruna Niyonzima
Midfielder

 • Full Name

  Haruna Niyonzima

 • Date of Birth

  February 5th, 1990

 • Place of Birth

  Rwanda

 • Height

  5 ft 5 1⁄2

 • Weight

  68 kg

Career

 • Goals: 5
 • Discipline: 3 fouls against
 • Passing: 23
 • Club Name: Simba Sports Club
 • Club Debut: May 24th, 2011
Simba Sports Club 0 Matches Played

Overview

Haruna Niyonzima ni kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Rwanda, ambaye takwimu zake zinaonyesha alizaliwa Februari 5, 1990, Gisenyi nchini Rwanda.

Alinza kucheza soka mwaka 2005, katika timu ya Etincelles, baadaye alihamia kwenye kikosi cha Rayon Sports ambapo alidumu hapo kuanzia mwaka 2006 hadi 2007.

Mwaka 2007 alihamia katika timu ya APR ambayo ni moja ya timu maaurufu na kubwa nchini Rwanda. alidumu hapo akiwa nahodha na mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda akiwa tegemeo katika safu ya kiungo cha ushambuliaji.

Mwaka 2011 alihamia Young Africans, klabu ambayo ni maarufu kwa jina la Yanga iliyopo Dar es Salaam, Tanzania.

Alianza kuichezea timu ya taifa ya Rwanda mwaka 2007, ameshaichezea timu yake ya taifa michezo 70.

Moja ya sifa yake kubwa awapo uwanjani ni kuwa mtaalam wa kuuchezea mpira na kupiga pasi za uhakika.

Nje ya soka Niyonzima ni mpenzi wa muziki na amewahi kusema kuwa anaweza kuimba muziki kwa ufasaha.

“Kiukweli napenda mpira ni kipaji lakini after football sometimes napenda kuimba naamini pia nikiingia naweza kuimba sababu nishawahi kufanya majaribio, nikisema nimejaribu kuimba ni kwamba nimeenda studio na sasa hivi na nyimbo kama tatu” aliwahi kunukuliwa akisema Niyonzima.

Niyonzima sasa ivi amesajiiwa na klabu Simba kwa mkataba wa miaka miwli 2017 mpaka 2019