Timu

Toto Africans Sports Club

Toto Africans Sports Club national

  • Established in

    1972

  • Manager Name

    18

  • Location

    Mwanza

CLUB HISTORY

Toto Africans Sports Club ni klabu ya michezo ambayo ipo jijini Mwanza, ilianzishwa mwaka 1972.

Haikuwa na umaarufu mkubwa miaka ya nyuma kwa kuwa kutoka Mwanza, timu iliyokuwa maarufu kipindi cha nyuma ni Pamba FC, hivyo kwa miaka mingi licha ya ushindani baina ya pande hizo bado Pamba ndiyo ambayo ilionekana kuwa na nguvu kuliko Toto katika mambo mbalimbali.

Umaarufu kwa Toto ulikua baada ya Pamba FC kuanza kupoteza mwelekeo na hivyo Toto ikawa na nguvu hatimaye ikapanda madaraja kutoka madaraja ya chini hadi Ligi Kuu Tanzania Bara.

HISTORIA YA TOTO
Toto Africans iliundwa na wakati wa Mwanza wakiwemo kina mzee Felician ambaye ndiye baba wa Fumo Felician, wengine ni Hamis Mabongo, Mombeki aliyekuwa meneja wa Sigara Mwanza, Amiri, Ally Yawanga na wengine wengi.

Toto ilitumia Uwanja wa Kirumba kwa ajili ya kufanya mazoezi, uwanja huo kwa sasa ndiyo Uwanja wa CCM Kirumba. Wakati huo ulikuwa ni uwanja wa wazi na Toto ilianzishiwa maeneo hayo.

Baadaye Toto ikahama Uwanja wa Kirumba ikahamia Uwanja wa Lake Sekondari ilikuwa ni kati ya mwaka 1974 hadi 1975 na uwanja huo kwa wakati ule ulikuwa ni wa wazi.

Mwaka 1977, Toto ilipambana ikatoka Ligi Daraja la Tatu hadi Ligi Daraja la Pili.

Baada ya kipindi hicho iliundwa timu nyingine ya Biashara ambapo wachezaji wengi wa Toto waliondoka wakakimbilia Biashara.

ilibidi viongozi wa Toto watumie nguvu kubwa kupambana timu yao isipotee. Waliendelea kuipambania na mwaka 2005 ikapanda daraja kucheza Ligi Kuu.

Kutokana na migogoro kadhaa, mwaka 2008, Toto ilishuka daraja, baada ya kujipanga upya tena, Toto ilirejea ligi kuu.

URAFIKI NA YANGA
Inatajwa kuwa Toto ni moja ya klabu ambayo imekuwa na ukaribu na Klabu ya Young Africans ‘Yanga’, kwa miaka mingi mashabiki wameamini hivyo kutokana na ukaribu wa viongozi baina ya pande hizo mbili.

TOTO vs SIMBA NI BALAA
Ukaribu huo umekuwa ukisababisha mchezo wa Toto dhidi ya  Simba kuwa mgumu kwa kuwa Simba ni wapinzani wa jadi wa Yanga.

Hivyo zinapokutana Simba na Toto mashabiki wamekuwa wakitafsiri ni kama Simba inacheza dhidi ya Yanga. Hiyo imechangia hata matokeo ya mchezo huo kuwa ambayo hayatabiriki.