Timu

Majimaji Football Club

Majimaji Football Club national

 • Established in

  1977

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Total Title

  3

 • Location

  Ruvuma

CLUB HISTORY

Majimaji Football Club ni klabu ya soka ambayo makao makuu yake yapo Songea mkoani Ruvuma.

Timu hii imekuwa ikitumia Uwanja wa Majimaji ambao una uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000.

Hii ni moja ya timu iliyapata umaarufu na kutamba katika miaka ya 1980 hadi 2000 mwanzoni,, ilipata umaarufu kutokana na kutoa wachezaji wengi wa kiwango cha juu waliofanikiwa kutamba miaka ya baadaye kuanzia ngazi ya klabu hadi timu ya taifa, Taifa Stars. Jina maarufu la Maji Maji ni Wanalizombe.

Historia, Majimaji ilianzishwa rasmi mwaka 1977 kwa muunganiko wa timu mbalimbali mjini Songea chini ya mwasisi wa timu hiyo, Dk Roulence Gama.

Ilianza kupata umaarufu mkubwa mwaka 1980 mwaka ambao timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

1980 Hadi 2001
Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mzee Gama alianzisha azimio la Mlale akiwa likiwa na maana ya kilimo pamoja na michezo.

Katika michezo aliweka nguvu zake katika soka ndipo akaanzisha timu ya Majimaji na kujenga Uwanja wa Majimaji, ambapo vyumba vyote vya uwanja huo aliwapangisha wachezaji wa Majimaji na kuwanunulia fenicha za ndani.

Majimaji ikiwa chini ya Abdallah ‘King’ Kibadeni alikuwa msaada mkubwa kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa. Majimaji ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Muungano mara mbili mfululizo mwaka 1885 hadi 1886.

Baada ya Gama kuhamishwa miaka ya 1990, Majimaji ilitetereka baada ya kuwa chini ya mkuu wa mkoa mwingine mzee Banduka ambaye alianzisha hoja ya timu kujiendesha yenyewe kibiashara.

Mwaka 1995, Banduka alihamishwa na nafasi yakeikachukuliwa na Anna Makinda.

Viongozi wa Majimaji walimfuata mkuu wa mkoa huyo mpya na kumweleza juu ya Azimio la Mlale ambalo liliasisiwa na mzee Gama na kuzaa timu hiyo.

Anna Makinda akakubali kubeba majukumu na akachangia kuinyanyua Majimaji kwa kusajili wachezaji wengi pamoja na kuwafungulia akaunti ya benki na kumwajiri kocha ambaye alimlipa shilingi laki 500,000 kwa mwezi.

Aidha, Makinda aliagiza kuwa kila mechi ambayo Majimaji itacheza, mapato ya uwanjani asilimia 70 yataenda kwa wachezaji wakishinda, sare asilimia 60 na wakifungwa asilimia 25.

Majimaji inaanza kufanya vizuri na ndipo mwaka 1996 ikashika nafasi ya nne katika ligi kuu, mwaka 1997 nafasi ya tatu na mwaka 1998, ikachukua ubingwa wa Ligi ya Muungano.

Baadhi ya wachezaji wa Majimaji wa kipindi hicho ni Shaib Kambanga, David Mjanja, Omari Kapilima, Godfrey Kikumbizi, James Mwagama, Stevin Mapunda, John Alex, Kelvin Haule na Doyi Moke.

Wengine ni Dello Ntumba, Omari Hussein, WIlle Martin, Said Msham, Samson Paul, Hamis Ngwena na Amri Said.

MIAKA YA 2000
Miaka ya 2000, Makinda aliondoka na nafasi yake ikachukuliwa na Said Said Kalembo, huyu haliiondoa Majimaji kwenye mipango yake na kusema klabu ijiendeshe yenyewe.

Licha ya juhudi kubwa ya kumuomba mkuu huyo wa mkoa kuendeleza utamaduni wa kuisaidia Majimaji bado maombo yao hayakukubalika. Hapo ikaanza kupotea mwelekeo. Mwaka 2001 ilishuka daraja.

KUSHUKA NA KUPANDA
Mwaka 2002 ilipanda daraja lakini mwaka 2005 ikarejea ilipotoka kutokana na mazingira magumu ya uendeshaji wa timu hiyo. Kuanzia hapo ikawa inapanda na kushuka mara kadhaa.

Kwa sasa Majimaji inashiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

1

Bingwa

Ligi ya Muungano

1985

1

Bingwa

Ligi ya Muungano

1986

1

Bingwa

Ligi ya Muungano

1998