Timu

African Sports Club

African Sports Club national

 • Established in

  1936

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Total Title

  1

 • Location

  Tanga

CLUB HISTORY

African Sports Club ini klabu ya michezo ambayo upo mkoani Tanga, timu ya soka ya African Sports imewahi kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara kadhaa.

African Sports ilianzishwa mwaka 1936 na maskani yake ni Barabara ya 12, Tanga, waasisi wake ni Mohammed Msuo, Mwajitu na Athumani Makalo.

Africans Sports ilishuka daraja mwaka 1991 na tangu hapo imekuwa ikipata wakati mgumu kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara.

African Sports iliwahi kubeba ubingwa wa Ligi ya Muungano mwaka 1988 uliozikutanisha timu za Tanzania Bara na Zanzibar ili kumpata bingwa wa jumla wa nchi na pia wawakilishi wa michuano ya Afrika.  

Wakati huo, bingwa wa Tanzania Bara ndiye aliyekuwa akishiriki katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, bingwa wa Ligi ya Muungano alikuwa anacheza Klabu Bingwa Afrika.

Mshindi wa pili wa Ligi ya Muungano, alikuwa anacheza iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi Afrika, baadaye ikaongezeka na mshindi wa tatu akawa anacheza Kombe la CAF.

Kwa sasa Kombe la CAF limeunganishwa na Kombe la Washindi na kuwa Kombe la Shirikisho wakati Klabu Bingwa Afrika imekuwa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ligi ya Muungano haipo kwa kuwa Zanzibar sasa ni mwanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), hivyo timu zake zinakwenda moja kwa moja kushiriki michuano ya Afrika.

Baadhi ya wachezaji walioipa jina African Sports miaka ya nyuma ni makipa Mohammed Yahya, Omar Mahadhi, mabeki Mweri Simba, Omar Zimbwe, Salim Kajembe, Muhaji Mwabuda na kiungo Amran Shiba.

African Sports ilichukua ubingwa wa Muungano ikiwa chini ya Kocha Syllersaid Mziray ‘Super Coach’ (marehemu), aliyekuwa akisaidiwa na Muhaji Mwabuda.

Baadhi ya wachezaji waliounda kikosi cha African Sports miaka ya 1970 ni; Salim Waziri, Bakari Tutu, Francis Mandoza, Hassan Banda, Mhando Mdevi, Raphael John, Abbas Mchemba, Twaha Omar, Victor Mkanwa, Mchunga Bakari na Juma Burhan.

Wengine ni; Duncan Mwamba, Martin Mahimbo ‘Water Green’, Abdul Ahmed ‘Bosnia’, Hamza Maneno na Dadi Fares.

Historia inaonyesha kuwa Mahimbo alipewa jina la Water Green na Twaha Omar kwa kuwa alichukua dawa ya kuchua misuli (Water Green) akaweka kwenye mswaki akidhani dawa ya meno.  

Makocha waliowahi kuifundisha timu hiyo ni; Charles Boniface Mkwasa na Freddy Felix Minziro.

Miaka ya hivi karibuni ilirejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msaada wa makocha Joseph Lazaro aliyewika Coastal Union na Yanga SC miaka ya 1990 na Kassim Mwabuda aliyechezea Mtibwa Sugar enzi zake.

Wachezaji ambao walipambana kuiwezesha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara ni Yussuf Abdul, Halfan Twenye, Mussa Ajiran, Juma Shemvuni, Mwaita Ngereza, Sultan Juma, Ramadhani Hamidu, Ally Ramadhani na Ally Shiboli.

Wengine ni James Mendi, Nyanda Kaziyoba, Tokala Nzau, Ayub Masoud, Ally Issa, Mussa Chambe, Ally Ahmed, Fadhili Kizenga, Evarstus Munjwahuki, Maulid Abbas, Nzara Ndaro, Rashid Ally, Hussein Issa, Zakaria Majaliwa, Issa Yassin, Paul Muna, Mohamed Rashid na Kassim Juma.


Mataji
Ligi ya Muungano 1988

1

Bingwa

Ligi ya Muungano

1988