Timu

Mbao Football Club

Mbao Football Club national

 • Established in

  2005

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Location

  Mwanza

CLUB HISTORY

Hii ni klabu ya soka ambayo inapatikana Kanda ya Ziwa, jijini Mwanza, inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2016/17 baada ya kupanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

ILIPANDA DARAJA KIBAHATI
Mbao FC ilipanda daraja licha ya kutokuwa katika timu zinazotakiwa kupanda daraja msimu wa 2015/16 kwa kuwa kuliibuka skendo ya upangwaji matokeo iliyozihusisha Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa.

Msimu huo, Mbao FC ilishika nafasi ya nne katika Kundi C hivyo kutokuwa na vigezo vya kupanda daraja lakini kwa kuwa timu za juu zilihusika katika skendo hiyo, ndipo nafasi ikawaangukia wao.

HISTORIA YA MBAO FC
Ilianzishwa mwaka 2005, waanzilishi ni wafanyabiashara wa biashara ya mbao ambao walikuwa wanafanya mazoezi jioni baada ya biashara zao.

Mwaka 2010 wakakubaliana kuisajili timu hiyo, mwaka huohuo baada ya kupata usajili ikashiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Ilemela 2010/11, haikufanikiwa kunyakua ubingwa. Ikashiriki ligi hiyo msimu uliofuatia wa 2011/12 ndipo ikafanikiwa kuwa bingwa.

Msimu wa 2012/13 ilishiriki Ligi Daraja la Tatu Mkoa, haikuchukua ubingwa. Msimu uliofuatia wa 2013/14 ikashiriki na kufanikiwa kuwa bingwa wa mkoa, hivyo ikashiriki katika Ligi ya Mabingwa Mikoa.

Mbao FC ilifanya vizuri na kupanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili, msimu wa 2014/15, ikafanya vizuri na kupanda hadi Ligi Daraja la Kwanza, ndipo ikapangwa Kundi C msimu wa 2015/16.

Timu hii imekuwa ikifanya mazoezi kwenye uwanja uliopo maeneo ya Sabasaba karibu la Soko Kuu la Mbao, lakini michezo yake ya nyumbani inacheza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba uliopo Kirumba, Mwanza.

UONGOZI WA MBAO FC
Mwenyekiti: Soli Zephania Nzashe
Makamu Mwenyekiti: Erick Gosso
Katibu Mkuu: Richard Athanas
Katibu Mipango: Yasin Abdul
Mweka Hazina: Bakari Mohamed
Ofisa Habari: Chricent Malinzi
Wajumbe wa Kamati Tendaji: Joseph Costantine, Bashir Khaleed, Leo Kambelembele, Philbert Magwisha

KIKOSI CHA SASA CHA MBAO FC
1. Hussein Swedy
2. Emmanuel Mseja
3. Steve Mganya
4. Steve Kigocha
 5. Asante Kwasi
6. Pius Buswita
7. Youssouf Ndikumana
8. Robert Magadula
9. Salmin Hoza
10. Emmanuel Mvuyekure
11. Dickson Ambundo
12. Erick Gwegwe
13. David Mwasa
14. Issack Issack
15. Frank Damas
16. Sameer Abeid
17. Venance Ludovic
18. Boniphace Maganga

BENCHI LA UFUNDI
Kocha Mkuu: Ettiene Ndaliyajige
Kocha Msaidizi:
Kocha wa Makipa: Soud Slim
Daktari wa Timu: Abdallah Chuma
Meneja wa Timu: Joseph Costantine
Mtunza Vifaa: John Kitanda