Timu

Mbeya City Council Football Club

Mbeya City Council Football Club national

 • Established in

  2011

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Location

  Mbeya

CLUB HISTORY

Agosti mwaka 2011, Rhino Football Club ya Arusha iliyokuwa ni klabu ya soka ilinunuliwa na mamlaka ya Jiji la Mbeya, hivyo timuhiyo ikabadilishwa jina na kuwa Mbeya City Council Football Club.

Hivyo ndivyo Mbeya City ilivyozaliwa na kuwa klabu ya soka iliyopo sasa.

Inamilikwa na mamlaka ya Jiji la Mbeya na ilipata jina kubwa kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa mara baada ya kupanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu Bara na kufanya vizuri katika ligi hiyo ikiwa na wachezaji ambao walionekana ni wa bei ya kawaida.

Mipango ya timu hiyo wakati ikibadilishwa jina na kubadilishwa umiliki ilikuwa ni kukuza mchezo wa soka jijini Mbeya na kutoa ajira kwa vijana.

Mbeya City Council Football Club maarufu kwa jina la Mbeya City FC imekuwa ikiongeza umaarufu kutokna a na aina ya uchezaji wake wa kutumia nguvu kubwa na upambanaji bila kujali kuchoka kwa muda wote.

Msimu wa 2013/2014, ndipo ambapo ilionyesha ‘maajabu’ kutokana na kucheza soka zuri ikiwa ndiyo kwanza imepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

Msimu huo timu hiyo ilicheza soka zuri na kuzisumbua Simba na Yanga ambazo ni timu kubwa katika ligi hiyo.

Mbeya City FC inaingiza mapato yake kupitia kwenye haki za matangazo ya AZAM TV, mapato ya mlangoni na kupitia wadhamini wa ligi kuu ambao ni Kampuni ya Vodacom Tanzania.

STAFU WA MBEYA CITY FC
Shah Mjanja
Mapigapicha

Mussa Mapunda    
Mwenyekiti

Emmanuel Kimbe
Katibu Mkuu

Joseph Semu    
Meneja Masoko

Frank Mfundo    
Meneja wa TMS


Dismas Ten
Ofisa Habari
MEDIA OFFICER

Joyce_Mwakifwamba    
Mwanachama


DANIEL EDWIN
Meneja Fedha