Timu

Mwadui Football Club

Mwadui Football Club national

 • Established in

  1970

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Location

  Mwanza

CLUB HISTORY

Hii ni timu inayoshiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo makao yake makuu yapo Mwadui mkoani Shinyanga.

Mwadui FC iliwahi kushiriki ligi hiyo miaka ya nyuma lakini iliposhuka daraja ililazimika kusubiri miaka 27 ili kufanikisha kurejea katika ligi kuu.

Ilitimiza lengo hilo baada ya kuifunga Burkifaso mabao 4-1 katika mechi ya mwisho ya Ligi Daraja la Kwanza iliyopigwa mwaka 2015 Kwenye Uanja wa Mwadui, Shinyanga.
Kocha aliyeiwezesha kurejea ligi kuu ni Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ambaye ni kocha na mchezaji wa zamani wa Simba.

Katika msimu ambao Mwadui ilipanda daraja ilipanda pamoja na Toto Africans ya Mwanza, Majimaji ya Songea na African Sports ya Tanga.

Baada ya kuongoza kwa miaka kadhaa, Julio alitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo katikati ya msimu wa 2016/17 kwa kile alichodai kuwa waamuzi kadhaa wanaionea timu yake na hawatendi haki pindi inapokuwa uwanjani ikicheza.

Baada ya Julio kuondoka, nafasi yake ilichukuliwa na Ali Bushiri huku kocha msaidizi akiwa ni Khalid Adam, daktari wa timu ni Shaban Shija, meneja wa timu ni Daud Ulaya, mtunza vifaa ni Nyakiage Jackson.

Mwadui FC inatumia Uwanja wa Mwadui Complex ambao upo maeneo ya Mwadui, Shinyanga kwa ajili ya mechi zake za nyumbani.