Timu

Mtibwa Sugar Football Club

Mtibwa Sugar Football Club national

 • Established in

  1988

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Total Title

  2

 • Location

  Morogoro

CLUB HISTORY

Hii ni klabu ya soka ambayo ilianzishwa mwaka 1988, kwa sasa inashiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ilianza kushiriki Ligi Daraja la Nne mwaka 1989, ikaendelea kucheza na kufanikiwa kupanda taratibu ngazi kwa ngazi, Mwaka 1996 ndipo ilipopanda daraja na kucheza Ligi kuu Tanzania Bara amayo kipindi hicho ilifahamika kwa jina la Ligi Daraja la Kwanza.

Inaumia viwanja viwili kama viwanja vyake vya nyumbani ambavyo ni Uwanja wa Jamhuri na Manungu vyote vipi mkoani Morogoro.

Inatumiwa Uwanja wa Manungu inapokuwa na mechi za kawaida zisizohusisha timu kubwa, inapokuwa inacheza dhidi ya Simba au Yanga huwa inahamia Uwanja wa Jamhuri kwa kuwa wapinzani wao hao wana idadi kubwa ya mashabiki, hivyo Uwanja wa Manungu ni mdogo na hauwezi kupokea idadi kubwa ya mashabiki.

Klabu hii inamilikiwa na Kiwanda cha Mtibwa Sugar Estates Ltd ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa sukari, pia kiwanda hicho ndicho ambacho kinamiliki timu ya Kagera Sugar ambayo nayo inashiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

KIKOSI CHA SASA
1. Benedict Tinoco
2. Rogers Gabriel
3. Issa Rashid
4. Kassim Ponera
5. Dickson Daudi
6. Shaban Nditi
7. Ally Makalani
8. Mohammes Issa
9. Rashid Mandawa
10. Haruna Chanongo
11. Ibrahim Rajab
12. Abdallha Makangana
13. Henry Joseph
14. Hussein Javu
15. Ally Shomari
16. Kelvin Friday
17. Said Bahanuzi
18. Ally Lundenga  

BENCHI LA UFUNDI
Kocha Mkuu: Zuberi Katwila
Kocha Msaidizi:
Kocha wa Makipa: Patrick Mwangata
Daktari wa Timu: Goodluck Mengi
Meneja wa Timu: Siddy Ibrahim
Mtunza Vifaa: Amir Abdallah

MAFANIKIO
Mwaka 1999 na mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo ikizipiku Simba na Yanga ambazo ndizo zilizokuwa zikitawala soka kwa miaka mingi nchini Tanzania.

1

Bingwa

TANZANIA PREMIER LEAGUE

1999

1

Bingwa

TANZANIA PREMIER LEAGUE

2000