Timu

Azam FC

Azam FC national

 • Established in

  2007

 • Club President

  Haruna Niyonzima

 • Manager Name

  Haruna Niyonzima

 • Total Title

  1

 • Location

  Dar-es-Salaam

CLUB HISTORY

Azam Football Club ni klabu ya soka ambayo ilianzishwa Juni 24, 2007, makao makuu yake yapo Chamazi jijini Dar es Salaam na kwa sasa inashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Azam ipo chini ya Bakhresa Group, hayo ni makampuni kadhaa ambayo yapo chini ya bilionea Said Salim Bakhresa.

Azam FC inamiliki uwanja wake wa Azam Complex ambao upo maeneo ya Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, uwanja huo ni maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamazi.

Uwanja huo una uwezo wa kuiongiza watu zaidi ya 5,000, pembeni ya eneo hilo la uwanja kuna viwanja vya mazoezi, bwana la kuogelea, gym pamoja na mabweni.

Azam FC ilianzia ngazi za chini katika ligi na ikafanikiwa kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu wa 2008–09. Msimu wa 2011–12 ikaweka rekodi ya kushika nafasi ya pili katika ligi kuu na kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho 2013, hayo yalikuwa mafanikio yao ya kwanza makubwa.

Baada ya muda kukawa na uwekezaji mkubwa klabuni hapo ambapo ikawa inasajili wachezaji wengi kwa dau kubwa, mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa dau kubwa ni Mtanzania Mrisho Ngassa, aliyesajiliwa akitokea Yanga.

Ngassa aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa zaidi na klabu ya soka ya Tanzania, inaelezwa ada yake ilifika zaidi ya shilingi milioni 98.

Azam FC pia iliwasajili Kali Ongala kutoka Sweden na Patrick Mafisango kutoka Rwanda. Mmmoja wa wachezaji ambaye amedumu klabuni hapo muda mrefu akitambulika kama ‘kijana wa nyumbani’ kutokana na kuanza kuichezea Azam FC tangu ikiwa ligi za chini ni John Raphael Bocco.

Azam FC iliweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara yao ya kwanza msimu wa 2013–14, ikimaliza pointi 6 juu dhidi ya Yanga ambayo ilishika nafasi ya pili.

KIKOSI CHA SASA
URAIA            NAFASI     MCHEZAJI
1. Tanzania      GK           Ally Mwadini
2. Tanzania      DF           Gadiel Mbaga Michael
3. Tanzania      MF           Shomari Kapombe
4. Zimbabwe    DF           Bruce Kangwa
5. Tanzania      DF           Erasto Nyoni
6. Tanzania      MF          Ramadhan Singano
7. Tanzania      MF          Salum Abubakar
8. Ghana         DF          Yakub Mohamed
9. Tanzania      MF          Joseph Mahundi
10. Ghana       FW         Yahaya Mohamed
11. Tanzania    DF           Daniel Amoah

12. Ghana         DF        Daniel Amoah
13. Tanzania    MF          Farid Marik
14. Tanzania    FW         Frank Domayo
15. Tanzania    FW         John Raphael Bocco
16. Tanzania    MF          Mudathir Yahaya
17. Tanzania    MF          Khamis Mcha
18. Tanzania    MF          Himidi Mao Mkami
19. Tanzania    FW         Ame Ally
20. Tanzania    DF          Abdallah Khery
21. Tanzania    DF          Waziri Omar
22. Cameroon  MF          Stephen Kingue
23. Tanzania    GK          Aishi Manula
24. Ghana       FW          Samuel Afful

UTAWALA
Mwenyekiti:     Abubakar Bakhresa (Tanzania)
Makamu Mwenyekiti: Nassor Idrisa (Tanzania)
Ofisa Habari:  Jaffar Idd Maganga

BENCHI LA UFUNDI
Kocha Mkuu: Aristica Cioaba (Romania)
Kocha Msaidizi: Idd Nassor Cheche (Tanzania)
Daktari wa Timu:  Juma Mwankemwa (Tanzania)
Meneja: Phillip Alando (Tanzania)
Kocha wa Makipa: Idd Aboubakar
Mtaalam wa Viungo: Saleh Jumapili
Mtunza Vifaa: Yusuf Nzawila

MAKOCHA WA AZAM FC
2008–09:         Neider dos Santos Brazil
2009–10:         Itamar Amorim Brazil
2010–12:         Stewart Hall England
2012:              Boris Bunjak Serbia
2012-13:         Stewart Hall England
2013-2014:      Joseph Omog Cameroon
2015-2016:      Stewart Hall England
2016:              Zeben Hernandez
2017-sasa:       Aristica Cioaba (Romania)

 

1

Bingwa

TANZANIA PREMIER LEAGUE

2014

1

Bingwa

KAGAME INTERCLUB CUP

2015