Timu

Simba Sports Club

Simba Sports Club national

 • Established in

  1936

 • Club President

  Evans Aveva

 • Manager Name

  Joseph Omog

 • Total Title

  32

 • Location

  Dar es Salaam, Tanzania

CLUB HISTORY

Simba Sports Club ni klabu ya michezo ambayo ndani yake kuna timu ya soka maarufu nchini Tanzania, makao makuu yake yapo Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Simba inashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uwanja wake wa nyumbani Uwanja wa Taifa pamoja na ule wa Uhuru, viwanja vyote hivyo vipo Dar es Salaam.

Simba ni wapinzani wakubwa wa Yanga, timu hizo ni kongwe na zina upinzani mkubwa wa jadi.

Simba ilipitia mchakato wa majina kadhaa kabla ya kutumia jina hilo la sasa, wakati klabu ikianzishwa mwaka 1936, ilitambulika kwa jina la Red, halikudumu muda mrefu ikaanza kujulikana kwa jina la Dar Sunderland, mwaka 1971 ndipo ambapo jina la Simba lilianza kutumika likimaanisha mnyama aina ya ‘lion’.

MAFANIKIO
Mafanikio makubwa ya Simba ni kucheza fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho inayoratibiwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) mwaka 1993, katika fainali hiyo Simba ilifungwa mabao 2-0 na Stella Club ya Ivory Coast (Côte d'Ivoire) kwenye Uwanja wa Uhuru ambao kipindi hicho ulijulikana kama Uwanja wa Taifa.

Yalikuwa mafanikio makubwa kwa Simba nje ya mipaka ya Tanzania. Mwaka 2003, Simba ilicheza robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) baada ya kuitoa Zamalek ya Misri ambayo ndiyo iliyokuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo.


KIKOSI CHA SIMBA CHA SASA 2016/17
     URAIA     NAFASI     MCHEZAJI
1. Ghana          GK         Daniel Agyei
2. DRC             DF         Javier Bokungu
3. Ghana          MF         James Kotei
4. Tanzania       MF         Mohamed Ibrahim ‘Mo’
6. Uganda        DF         Murshid Juuko
7. Tanzania       FW         Haji Ugando
8. Tanzania       MF         Mwinyi Kazimoto
10. Tanzania     FW         Juma Luizio
11. Burundi      FW         Laudit Mavugo
13. Tanzania     MF         Saidi Hamisi Ndemla
14. Tanzania     MF         Jamal Mnyate
15. Tanzania     DF         Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jnr’
16. Tanzania     FW         Pastory Athanas
17. Zimbabwe   DF         Method Mwanjale
19. Tanzania     MF         Mzamiru Yasin
20. Tanzania     MF         Jonas Mkude (captain)
21. Tanzania     DF         Novaty Lufunga
22. Tanzania     GK         Manyika Peter
23. Tanzania     MF         Ibrahim Ajibu
24. Tanzania     DF         Abdi Banda
25. Tanzania     MF         Shiza Ramadhani Kichuya
27. Ivory Coast  FW        Fredrick Blagnon

BENCHI LA UFUNDI
Kocha Mkuu: Joseph Omog (Cameroon)
Kocha Msaidizi: Jackson Mayanja (Uganda)
Kocha wa Makipa: Abdul Idd Salim (Kenya)
Daktari wa Timu: Yassin Gembe (Tanzania)
Mratibu wa Timu: Abbas Suleiman Ally (Tanzania)
Meneja wa Timu: Mussa Hassan Mgosi (Tanzania)
Mtunza Vifaa: Hamis Mtambo(Tanzania)

MCHEZAJI ALIYEFANIKIWA
Mbwana Samatta ni Mtanzania ambaye aliwahi kuichezea Simba kwa msimu mmoja mwaka 2011, alionyesha uwezo wa juu na hiyo ikasababisha asajiliwe na TP Mazembe ya DR Congo.

Alicheza TP Mazembe kisha mwaka 2016 akasajiliwa na Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Ndani ya muda mfupi amekuwa na mafaniki kikosini hapo na ni mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Genk.

MAKOCHA WA SIMBA TANGU MWAKA 1998 HADI SASA

Mwaka

Jina

 Nchi

 

1998

Mohamed Kajole

Tanzania (marehemu)

1999

David Mwamaja

Tanzania

2000

Nzoyisaba Tauzany

Burundi (marehemu)

2000

Abdallah Kibaden

Tanzania

2000

Syllersais Mziray

Tanzania (marehemu)

2001

James Siang’a

Kenya

2005

Patrick Phiri

Zambia

2006

Neider dos Santos

Brazil

2007

Talib Hilal

Tanzania

2010

Milovan Cirkovic

Serbia 

2010

Patrick Phiri

Zambia

2011

Krasmir Benziski

Bulgaria

2012

Moses Basena

Uganda

2012

Milovan Cirkovic

Serbia

2012

Partick Liewing

France

2013

Abdallah Kibaden

Tanzania

2013/4

Zdravko Logarusic

Croatia

2014

Patrick Phiri

Zambia

2015

2015 - Januari 12, 2016

Goran Kopunovic

Dylan Kerr

Serbia

England

2016 Januari 13

Jackson Mayanja (care taker)

Uganda

2016-sasa

Joseph Omog

Cameroon

18

CHAMPION

TANZANIA PREMIER LEAGUE

1965, 1966 (as Sunderland) 1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1993, 1994, 1995, 2001, 2002, 2004, 2007, 2009–10, 2011–12

3

CHAMPION

TANZANIA CUP

1984, 1995, 2000

5

CHAMPION

TANZANIA TUSKER CUP

2001, 2002, 2003, 2005 2005 (in Kenya)

0

FINALIST

CAF CUP

Finalist: 1993

6

CHAMPION

CECAFA CLUB CUP

1974, 1991, 1992, 1995, 1996, 2002

Home Kit

Away Kit