Habari za Kitaifa

WAZIRI MWAKYEMBE KUWAPOKEA SERENGETI BOYS 

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 18, Serengeti Boys, inatarajia kutua nchini Alfajiri ya kesho (May 1) huku ikilakiwa na Waziri mwenye dhamana ya Michezo sanaa na burudani Dk Harison Mwakyembe.

Timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa vijana wa CECAFA kwa wachezaji wenye umri huo, awali ilifahamika kama watatua nchini Alfajiri ya juma tano, lakini CECAFA wamewabadilishia tiketi na hiyo kutua Alfajiri ya Jumanne (Kesho) majira ya saa tisa Alfajiri kupitia shirika la ndege la Rwanda.

Serengeti Boys wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo jana (April 29), baada ya kuwaduwaza Somalia katika mchezo wa fainali kwa jumla ya mabao 2-0.