Habari za Kitaifa

NIYONZIMA YUPO TANZANIA, MASHABIKI WAMSUBIRI KWA HAMU UWANJANI

Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima kupitia taarifa rasmi kutoka kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara amethibitisha kuwa mchezaji huyo yupo nchini.

Niyonzima amekuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kuwa majeruhi ambapo awali ilielezwa alihitaji upasuaji baada ya mfupa wa mguu wake kugundulika kuwa ulikuwa na ufa wa muda mrefu.

Alisafiri hadi India kwa ajili ya zoezi hilo lakini madaktari wa India wakampatia tiba mbadala iliyotatua tatizo lake na kumfanya arudi katika hali yake ya kawaida pasipo kuhitaji kufanyiwa upasuaji.

Baada ya taarifa hiyo kumekuwa na maoni mengi kutoka kwa mashabiki wa Simba wakihoji atarejea lini uwanjani kuitumikia timu yake hiyo.