Habari za Kitaifa

YANGA MAMBO SAFI, WALAMBA MKATABA WA BILIONI 2

 Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa miaka mitatu na Kampuni Ya utengenezaji wa Vifaa vya Michezo ya Macron ambayo makao makuu yake yapo nchini Italia.

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema mkataba huo unathamani ya shilingi bilioni mbili ambapo kutakuwa na ongezeko la asilimia kila mwaka kutokana na mauzo ya jezi na vifaa mbalimbali.

Kutokana na makubaliano hayo inamaanisha, Macron watakuwa ndiyo wanakuwa watengenezaji wakuu wa vifaa vyote michezo vya klabu hiyo.

Mwakilishi wa Kampuni ya Macron Tanzania Suleyman Kareem amesema, wamevutiwa na Yanga kwa sababu ni klabu nchini hivyo itakuwa vizuri kufanya kazi na klabu hiyo.