Habari za Kitaifa

STRAIKA MAJIMAJI ALIA NA UWANJA WAO, ASEMA UNAWAKWAMISHA

Wiki chache tangu Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru anukuliwe akisema kuwa timu yake imekuwa ikipata matokeo ambayo siyo mazuri inapokuwa nyumbani kutokana na uwanja wao, kuna mwingine naye ameibuka.

Ndunguru alinukuliwa akisema kuwa uwanja wao wa Majimaji uliopo Songea umekuwa ukiwapa wakati mgumu wachezaji wao na ndiyo maana wanapotoka nje wa Songea wanacheza soka zuri kuliko wakiwa nyumbani.

Mshambuliaji wa timu hiyo, Marcel Boniventure ambaye ana mabao matatu katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2017/18 naye amesema kuwa uwanja huo kuna wakati unawapa wakati mgumu wa kufanya vizuri vile wanachokipanga.

Boniventure alisema hayo baada ya mchezo wao dhidi ya Stand United ambapo alifunga bao moja la ushindi.

Uwanja wa nyumbani hauna ubora mzuri, kuna wakati unajipanga kufanya kitu fulani, lakini kutokana na uwanja mambo yanakuwa yanaenda ndivyo sivyo,” alisema mshambuliaji hiyo.