Habari za Kitaifa

JERRY MURO: “YANGA MNAWASAJILI WACHEZAJI DHAIFU HAWAENDANI NA UKUBWA WA KLABU”

Baada ya uongozi wa Yanga kumtambulisha kiungo Mohamed Issa ‘Banka’ kuwa imemsajili kwa mkataba wa miaka miwili, aliyekuwa ofisa habari wa klabu hiyo Jerry Muro amekosoa usajili huo.

Muro alitoa maoni yake hayo kwenye ukurasa wa Instagram ya Yanga baada ya klabu hiyo liweka picha ya Banka akiwa amevaa jezi ya Yanga.

“Hapa ndipo napojiuliza haya mambo yataisha lini awali tuliambiwa usajili ni kimyakimya, sasa naona mmeanza kutoa hadharani, haya tuendelee kuweka wengine hadharani.”

“Ila bado mnawasajili wachezaji dhaifu sana ambao hawaendani hadhi ya klabu kubwa kama Yanga. Hawa wachezaji wamechoka sana hawana tena uwezo, pumzi, akili na mbinu mpya hawa wanaelekea ukingoni mwa uchezaji wao.”

“Nawashauri Yanga hawa wachezaji mnasajili kwa ajili ya Yanga Veterans tu.”