Habari za Kitaifa

YANGA YASHUSHA MASHINE KUTOKA MTIBWA SUGAR, YADONDOKLA MIAKA MIWILI

Baada ya ukimya wa muda, hatimaye Yanga nayo imeonyesha makucha, hiyo ni baada ya kumtambulisha Mohammed Issa 'Banka' kujiunga na timu hiyo. 

Banka ambaye ni kiungo, amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.

'Mo Banka' ametambulishwa leo Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh aliyeambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam.

Nyika amesema kwamba Mohamed Issa 'Banka' ni mchezaji mzuri na wameridhika na kiwango chake ndio maana wamemsajili na kumpatia mkataba wa miaka miwili.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh (kushoto) akiwa na kiungo mpya, Mohammed Issa 'Banka' na Mwenyekiti wa Usajili, Hussein Nyika