Habari za Kitaifa

MTIBWA YAITOA NISHAI SIMBA, YATINGA FAINALI, KUIVAA STAND UNITED

mtibwasugar

Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya vijana ya Kombe la Uhai baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo uliopigwa leo jioni.
Mtibwa Sugar imetinga fainali kwa kuichapa Simba kwa bao 1-0 katika mtanange uliopigwa jijini Dodoma.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar itakutana na Stand United ambayo nayo imetinga fainali kwa kuifunga Azam FC bao 1-0.