Habari za Kitaifa

ZFA YAENDELEA KUMOMONYOKA

YANGAVSMBAO

Mwandishi Wetu, Pemba

HATIMAYE sinema ya kujiuzulu kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA) imeendelea ambapo Makamu wa Rais wa ZFA Pemba, Ali Mohammed Ali, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo.

Makamu huyo ameungana na Rais wa chama hicho, Ravia Idarous Faina, Makamu wa Rais Unguja, Mzee Zamu Ali na Abdul Ghani Msoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, makamu huyo alisema hatua hiyo imekuja baada ya kujitathimini kwa kina na kuona tayari viongozi wenzake wameshaachia ngazi nyadhifa zao.

WhatsApp Image 2018 06 14 at 6.30.27 AM

“Baada ya kuona viongozi wenzangu wa juu wamejiuzulu nyadhifa zao, sina budi na mimi kujiuzulu kama walivyofanya wenzangu, kuanzia leo tarehe 13/6/2018,” alisema.

Katika hatua nyingine, kigogo huyo amesema yupo tayari kushirikiana na viongozi wapya wa chama hicho endapo akitakiwa kufanya hivyo ili kuhakikisha soka la Zanzibar linapiga hatua.