Habari za Kitaifa

PLUJIM AMPA JUMA MWAMBUSI ULAJI AZAM

Screen Shot 2018 06 12 at 8.19.11 PM

KOCHA mkui wa Azam FC, Hans van Plujim, ni kama amempa shavu aliyekuwa msaidizi wake katika kikosi cha Yanga Juma Mwambusi baada ya kumjumuisha katika benchi la Azam kama kocha wake msaidizi.

Mwambusi aliyewahi kukinoa kilosi cha Mbeya City kabla ya kuwa msaidizi wa Plujim ndani ya Yanga, sasa ndiye atakuwa msaidizi wa Plujim katika kikosi cha Azam kwa msimu ujao wa 2018-19.

Akizungumza na Magic FC, meneja wa Azam FC alikiri kumpa kocha huyo kandarasi ya miaka miwili na kuweka wazi kuwa Mwambusi na Iddy Cheche wote watakuwa wasaidizi wa mholanzi huyo.

"Uwezo wa Mwambusi unajulikana na huu ni wakati muafaka wa kufanya tena kazi na Plujim kama walivyokuwa Yanga na lengo letu ni kuhakikisha Azam tunakuwa vizuri kwa msimu ujao"

"Wasaidizi siyo lazima awe mmoja, wanaweza kuwa hata wanne hivyo kocha wetu Cheche bado yupo na Mwambusi anaongezeka hivyo wote watakuwa chini ya Hans van Plujim" alisema Alando.

Mwambusi atakumbukwa kwa kikosi cha Mbeya City kilichowahi kufanya vizuri pindi walipopanda daraja misimu mitatu iloyopita.