Habari za Kitaifa

SIMBA WAPEWA MAPUMZIKO KUREJEA NA STAIKA WA KIGENI

Screen Shot 2018 06 12 at 10.21.00 AM

UONGOZI wa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC, umewapa mspumziko ya muda mfupi wachezaji na benchi la ufundi ikiwa ni baada ya tuzo za Mo Simba awards zilizotolewa jana Juni 11.

Akizungumza na Radio E fm, msemaji wa klabu hiyo Haji Sunday Manara, aliweka wazi hayo huku akisisitiza kuwa wataongeza mshambuliaji mmoja wa kimataifa ili kukipa nguvu kikosi hicho.

Manara ambaye ni mshindi wa tuzo ya muhamasishaji bora wa mwaka ndani ya Simba, aliyasema hayo huku akigoma kusema mchezaji huyo wa kigeni anatokea nchi gani huku akisema kuwa hakuna mchezaji hata mmoja Afrika Mashariki hii anayeweza kutakiwa na Simba akakataa.

"Tumewapa mapumziko vijana wetu na watarejea kujiandaa na michuano ya Kagame itakayoanza mwishoni mwa mwezi huu hapa jijini na tumejipanga kupambana"

"Tunachokitaka ni kuhakikisha kuwa tunapambana na tutafanya usajili wa mchezaji wa kigeni atakayeongeza nguvu katika nafasi ya ushambuliaji na niseme tuu kuwa tutapeleka kikosi kizima kwakuwa tunahitaji kombe hilo" alisema Haji Manara.

Simba ilishindwa kuibuka wababe katika michuano ya Sportpesa huku wakishindwa kufunga bao lolote katika michezo mitatu huku wakikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa wa Ligi kuu nchini Kenya Gor Mahia.