Habari za Kitaifa

MO DEWJI AKUBALI KUNUNUA HISIA ZA SIMBA KWA 49%, MAMBO YANAENDA VIZURI

Habari ni kuwa Mohammed ‘Mo’ Dewji amekubali kununua asilimia 49 za hisa za Klabu ya Simba kama maelekezo ya serikali yalivyo.

Mwanasheria wa Simba, Evodius Mtawala ameyazungumza hayo leo aliozungumza na wanahabari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mtawala amewataka wanachama wa Simba kujitokeza kwa wingi katika Mkutano wa mabadiliko ya Katiba utakaofanyika Mei 20, mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo eneo la Ocean Road mjini Dar es Salaam.

Mkutano huo ulioitishwa na Kaimu Mwenyekiti, Salim Abdallah ‘Try Again’ unatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na tayari wanachama wamekwishasomewa ajenda kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya klabu hiyo, kufungu cha nne.