Habari za Kitaifa

FULL TIME: SIMBA 2-0 TANZANIA PRISONS ‘LIVE’ UWANJA WA TAIFA, LIGI KUU YA VODACOM

FULL TIME

Mchezo umemalizika

90' Zinaongezwa dakika tatu za nyongeza.

86' Okwi anatoka anaingia Laudit Mavugo.

83' Prisosn wanafanya mabadiliko, anatoka Sungura anaingia Chudu.

Simba wanapata bao la pili kwa penati, Okwi anamhamisha kipa wa Prisons.

Gooooooooooooooooooooo

Okwi anaenda kupiga.

El Fadhil anapata kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya Bocco, inakuwa penati.

76' Bado Simba wanaongoza bao 1-0.

72' James Kotei kaingia kuchukua nafasi ya Asante Kwasi.

68 Simba wanashambulia, Kichuyta anawavuruga walinzi wa Pirsons lakini anashindwa kumalizia kazi.

67' Kwasi ameumia anatolewa nje kutibiwa. 

57' Jonas Mkude anapata kadi ya njano kwa kucheza vibaya.

56' Simba wanapata faulo, Okwi anapiga mpira unapaa juu ya lango. 

49' Shambulizi kali langoni mwa Prisons, mpira unatoka nje.

48' Simba wanapata kona tatu mfulizo.

46' Simba wanaanza kwa kasi.

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

45' Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.

44' Simba wanapata faulo, anapiga Kichuya, alamnusura iwe bao.

43' Simba wanaanza mashambuzlizi kutokea nyuma, Jonas Mkude anatawala eneo la katikati.

38' Simba wanaongeza kasi ya kushambulia.

Simba wanapata bao kupitia kwa John Bocco, alimalizia kazi nzuri ya Erasto Nyoni, krosi iligonga nguzo ikarejea, Bocco akamalizia kwa kichwa.

35' GOOOOOOOOOOOOOOOOOO

34' Simba wanapata kona, ni kona yao ya sita.

30' Okwi anafanya shambulia kali lakini beki wa Prisons ana ublock mpira, anatoa pasi kwa Kichuya lakini naye anashindwa kufunga.

29' Mchezo unaendelea.

28' Jezi namba 27 wa Prisosn yupo chini, ameumia, mchezo umesimama kwa muda anatibiwa. Ametolewa nje kwa machela.

22' Simba wanapata kona, ni ta tano kwao katika mchezo huu.

16' Simba wanatengeneza shambulizi kupitia pembeni.

15' Juuko na Kapombe wanapigiana pasi kwa umakini.

10' Prisons wanaonyesha kuwa makini muda mwingi.

7' Simba ndiyo wanamiliki mpira muda mwingi.

4' Timu zote zinasomana  taratibu, hali ya hewa ya kibaridi kinatawala hapa uwanjani. 

2’ Kona inapigwa inatolewa na walinzi wa Prisons.

1’ Shiza Kichuya wa Simba anafanya shambulizi inakuwa kona.

Mchezo umeshaanza.

Huu ni mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom, unapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Simba

1. Aishi Manula

2. Shomary Kapombe 

3. Mohammed Hussein

4. Juuko Murshid

5. Yusuph Mlipili

6. Erasto Nyoni 

7. Shiza Kichuya 

8. Jonas Mkude

9. John Bocco

10. Emmanuel Okwi 

11. Asante Kwasi

 Wachezaji wa akiba

 12. Said Mohamed

13. Nicholas Gyan 

14. Paul Bukaba 

15. James Kotei 

16. Mzamiru Yassini

17. Rashid Juma