Habari za Kitaifa

MVUA YA DAR, NEEMA KWA PRISONS, YATAMBA KUIPIGA SIMBA, LEO NDANI YA UWANJA WA TAIFA

Leo Jumatatu Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kwenye Uwanja wa Taifa ambapo  Tanzania Prisons watakuwa wageni wa vinara wa ligi hiyo, Simba, licha ya kuwa ugenini, Simba wamejinadi kuwa watafanya kweli tokana na hali ya hewa ya Dar kwa sasa kuwa rafiki kwao.

Jiji la Dar kwa sasa limekuwa likikabiliw ana mvua nyingi kwa siku kadhaa, hadi leo Jumatatu mvua zimeendelea kunyesha katika maeneo mengi ya jiji hilo.

Meneja wa Tanzania Prisons, Havitishi Abdallah amefunguka kuwa wanaamini katika mchezo huo wa leo wataonyesha uwezo wa juu.

 “Tunataka tuwaambie Simba hii ni Prisons wasitufananishe na timu nyingine, sisi tutawafanyia kitu kibaya waamini hivyo kwa sababu tupo vizuri sana na hii hali ya hewatunapenda iwe hivihivi kwa sabbau tukikutana hali yetu ya hewa kama hii inakuwa burudani.”

“Hatuiogopi Simba ni kama timu nyingine tulizokutana nazo ni kweli wana jina kubwa na tuna waheshimu wapo juu lakini hiyo haitutishi, wana mwalimu mzuri na sisi tuna mwalimu mzuri ndiyo maana najiamini.”

Prisons itawakosa wachezaji wake watatu katika mchezo wao dhidi ya Simba, Laurent Mpalile, Kassim na Sabianka ambao wana matatizo, wachezaji wengine wapo vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.