Habari za Kitaifa

BAADA YA USHINDI! YANGA WAKWEA PIPA USIKU KUELEKEA BOTSWANA

 

Muda mfupi baada ya kuifunga Stand United mabao 3-1, Yanga iliondoka usiku wa jana kuamkia leo kuelekea Botswana tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers.

Yanga wameenda Botswana wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, hivyo wanahitaji ushindi wa bao 1-0 ili kusonga mbele kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo wa jana dhidi ya Stand, Yanga ilicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza wkati Stand walichachamaa kipindi cha pili lakini hawakuweza kubadili matokeo.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Ibrahim Ajib, bao la kujifunga kwa beki wa Stand United, Ali Ali na Obrey Chirwa huku Vitalis Mayanga akifunga bao la kufutia machozi kwa Stand.