Habari za Kitaifa

YANGA 4-1 MAJIMAJI ‘LIVE’, FULL TIME, UWANJA WA TAIFA

FULL TIME

Mchezo umefikia tamati.

Dakika ya 90: Zinaongezwa dakika 3.

Dakika ya 85: Nadir Cannavaro anaingia, anatoka Andrew Vincent Dante kwa Yanga.

Yanga wanapata bao la nne, Tshishimbi anapiga shuti kali.

Dakika ya 83: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 70: Majimaji wameamka na kuwabana Yanga.

Dakika ya 67: Mchezo umepungua kasi, Majimaji wamechangamka tofauti na kipindi cha kwanza.

Dakika ya 60: Majimaji wamepata uhai. Wanaonyesha kupambana.

Dakika ya 56: Majimaji wanapata bao la kwanza, mfungaji ni Marcel Bonivanture, anafunga kwa penati.

Dakika ya 55: Said Makapu anaunawa mpira inakuwa penati.

Dakika ya 51: Majimaji wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwa mpigo.

Dakika ya 47: Bonivanture anakaribia lango la Yanga lakini walinzi wanakuwa makini kuzmuia.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Dakika ya 45: Inaongezwa dakika moja ya nyongeza.

Martine alipiga shuti kali kutoka nje ya eneo la 18 mpira uanignia wavuni.

Dakika ya 43: Yanga wanapata bao la tatu, linafungwa na Emmanuel Martine.

Dakika ya 42: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 39: Buswita wa Yanga anapiga shuti linagonga nguzo na kurejea uwanjani.

Dakika ya 33: Majimaji mambo magumu, wanaonekana kuzidiwa.

Dakika ya 29: Chirwa anaipatia Yanga bao la pili, akimalizia kwa kichwa krosi ya Gadiel Michael.

Dakika ya 25: Yanga wanafanya shambulizi kali.

Dakika ya 20: Yanga sasa wanamiliki mpira na kupata shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki wao.

Kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi anapiga kupiga penalti, anafunga.

Mpoki Mwakinyuke wa Majimaji anapewa kadi nyekundu kwa kuushika mpira makusudi ndani ya eneo la 18.

Dakika ya 17; Yanga wanapata penalti, Chirwa anaiwezesha Yanga kupata penalti.

Dakika ya 10: Mchezo umeanza kuwa na kasi. Yanga wanatawala muda mwingi.

Dakika ya 8: Majimaji wanajipanga.

k ya 2: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.

Mchezo umenza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom