Habari za Kitaifa

MGHANA WA AZAM FC HOI, STRAIKA NAYE KUPIGWA KISU KWENYE MGUUNI 

Wakati nahodha wa Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’ akiwa njiani kuelekea jijini Cape Town, nchini Afrika Kusini, kesho Alhamisi kufanyiwa uchunguzi wa goti la mguu wake kulia linalomsumbua, kuna ‘majanga’ mengine ndani ya timu hiyo.

Daktari Mkuu wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Wazir Junior, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo wa mguu Moi baada ya donge la damu kuvilia chini ya mguu.

“Wazir (Junior) alikuwa na tatizo kwenye kifundo cha mguu na tumemfanyia vipimo vyote vya M.R.I, X-Ray, alikuwa akitibiwa Moi sasa hivi taratibu zinafanyika matibabu ya zaidi yatakuwa katika Hospitali ya Moi, ambayo atafanyiwa upasuaji mdogo baada ya kujulikana kuwa chini ya mguu kuna bonge la damu kwa hiyo tunatarajia ndani ya siku mbili hizi Junior kufanyiwa upasuaji huo,” alisema.

 

Amoah uchunguzi

Akizungumzia matibabu ya beki Daniel Amoah, anayesumbuliwa na maumivu ya goti, alisema kuwa wanatarajia kufanya taratibu za kumfanyia kipimo cha M.R.I na kuangalia tatizo linalomkabili ndani ya goti hilo.

“Mtakumbuka siku ya mechi yetu na Stand United alianguka kandokando ya kiwanja na kujiumiza lakini tulikuwa tukimuuguza na kumpatia dawa akapata nafuu akacheza mechi ya Simba, lakini baada ya mechi ya Simba yale maumivu yamejirudia tena na sasa tunafanya taratibu za kumfanyia kipimo cha M.R.I…na baada ya kupata majibu ya M.R,I tutawafahamisheni zaidi ni jinsi gani matibabu yake yatakuaje,” alisema.