Habari za Kitaifa

ZITTO KABWE ATUA UBELGIJI KUMSALIMIA MBWANA SAMATTA

 

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa Facebook kuelezea juu ya safari yake ya nchini Ubelgiji ambapo pia amepata nafasi ya kusalimiana na mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta.

Nimepita Kumsabahi Nahodha Samatta - Zitto

Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.

Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi. 

Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto

Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo 

Genk 

Ubelgiji 

Februari 13, 2018