Habari za Kitaifa

SIMBA SAFARINI SHINYANGA KUWAFUATA MWADUI FC

 

Baada ya kuonyesha makali katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, sasa Simba inarejea kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

Simba inarejea kwenye ligi hiyo ambapo inatarajiwa kusafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa timu hiyo itaondoka Dar Jumanne ya wiki hii kwa ajili ya kipute hicho ambacho kitapigwa Alhamisi ya wiki hii.