Habari za Kitaifa

BAADA YA BAO DHIDI YA KAGERA SUGAR, SAID NDEMLA ALA SHAVU LINGINE

 

Baada ya kiungo Said Ndemla wa Simba kufunga bao moja na kuiwezesha timu yake kushinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, mchezaji huyo alipata shavu la kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi na Mashabiki wa Simba.

Ofisa wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa bao hilo na kiwango kizuri ambacho amekionyesha jana Jumatatu, kimemfanya Ndemla achaguliwe kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mchezaji Bora wa Mechi katika huduma ya SimbaApp.