Habari za Kitaifa

VAN PLUIJM ASHUKURU KUTEULIWA KUWA KOCHA BORA

Kocha Mkuu wa Singida United, Hans van der Pluijm ameishukuru kamati ya Kombe la Mapinduzi kwa kumteua kuwa kocha wa kikosi bora cha michuano hiyo iliyomalizika jana usiku.

Pluijm amesema hiyo ni heshima kubwa kwake na anawathamini wale wote ambao wameuona uwezo wake na kuamua kumteua yeye kuwa kocha bora wa timu hiyo.

“Ni furaha kwangu na hii inaonyesha namna gani kwamba wanatambua kile ninachokifanya tangu nimekuja Tanzania na kuanza kushiriki michuano hii nikiwa na Yanga na sasa Singida United," alisema Pluijm.

Kocha huyo amesema ataendelea kufanya vizuri zaidi na zaidi katika mwaka ujao akiwa na timu hiyo na kile walichokionyesha mwaka huu ni mfano lakini msimu ujao atakuja kwa lengo la ubingwa na siyo kingine.