Habari za Kitaifa

DARAJA LA KWANZA UWANJANI WIKIENDI HII, TIMU YA KOCHA JULIO KAZI IPO

Baada ya sekeseke la wiki moja na vijembe vya hapa na pale kwa timu zinazoshika nafasi za juu katika Ligi Daraja la Kwanza katika Kundi C hali iliyosababisha kufungiwa kwa

waamuzi wa mchezo wa Dodoma FC dhidi ya Alliance uliochezwa Desemba 30, mkoani Dodoma, sasa moto wa ushindani utaendelea kuwashwa mwishoni mwa wiki hii kwa timu zote kuingia dimbani.

Katika Uwanja wa Alhasan Mwinyi Pale mkoani Tabora kutakuwa na mchezo kati ya wanajeshi Rhino ambao watakuwa wenyeji wa Dodoma FC ambayo inanolewa na Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Shughuli pevu ikiwa katika Dimba la Kumbukumbu ya Karume mkoani Mara wilayani Musoma ambapo Biashara FC watawakaribisha Alliance School ya jijini Mwanza.

michezo hiyo inatarajiwa kuteka hisia za mashabiki wengi wa Soka la Tanzania kutokana na uwiano wa Alana katika Kundi C ambapo Dodoma FC wanaongoza wakiwa na jumla ya alama 21, Biashara FC wakiwa katika nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 20 huku Alliance ikiwa katika nafasi ya tatu na jumla ya alama 19.

Katika hatua Nyingine timu ya Toto Africans itapambana kukipiga dhidi ya JKT Oljoro katika mchezo wao utakaopigwa Jumamosi ya Januari 13 kwenye Uwanja wa Nyamagana, Toto iko mkiani mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 8 katika michezo 10, nyuma ya Transit Camp na Rhino.

Aidha, Pamba au TP Lindanda watashuka uwanjani keshokutwa Jumapili, Transit Camp.