Habari za Kitaifa

MKE WA MKWASA AMJIA JUU BWANA SHAMBA OBREY CHIRWA

 

Muda mfupi baada ya Yanga kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, kukaibuka maneno mengi juu ya mchezaji wa timu hiyo, Obrey Chirwa ambaye alikosa penati na kuifanya Yanga kutolewa kwa matuta 5-4.

Chirwa ambaye alikuwa kwao Zambia kutokana na mgogoro kati yake na uongozi wa klabu yake, muda mwingi aliutumia akiwa shambani akifanya kazi za ukulima kama ambavyo yeye mwenyewe alivyokuwa akiposti katika mitandao ya kijamii.

Sasa baada ya kukosa penati katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya URA kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, lawama zimekuwa nyingi juu ya mchezaji huyo ambaye baadhi ya mashabiki wanamuita ‘MKULIMA’ au BWANA SHAMBA’

  Mke wa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, anayejulikana kwa jina la Beatrice Chalamila maarufu kwa jina la Betty Mkwasa naye ni mmoja wa waliomtupia lawama Chirwa kutokana na kile kilichotokea.

Wachezaji wengine wa Yanga ambao walipiga mikwaju yao na kupata ni Papy Kabamba Tshishimbi, Hassan Ramadhani Kessy, Raphael Daudi Lothi na Gardiel Michael Mbaga.

kwenda kuchukua nafasi ya Pius Buswita dakika ya 53 kungeiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ya Yanga, lakini Mzambia huyo alishindwa kucheza vizuri kutokana na kile kilichoonekana wazi hakuwa fiti.

Akizungumzia mchezo huo, kupitia ukurasa wake wa Facebook, Betty Mkwasa alisema: “Yaani ni kama Yanga walicheza pungufu uwanjani. Hakuwa na msaada wowote. Wakati fulani tuweke kando ushabiki tuzungumzie soka letu.” 

“Angalia (Donald) Ngoma yuko wapi, angalia (Thabani) Kamusoko, ndiyo walewale wenye migomo baridi. Tuache kusajili mapro kwa kushindana na Simba na Azam wenye fedha zao, tuwatumie yosso na wazalendo wetu ambao hadi sasa wameonyesha uwezo mkubwa,” alisema Betty.