Habari za Kitaifa

TPLB YANOGESHA ZAWADI YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI VPL

Bodi ya ligi (TPLB) imeikishirikiana na wadhamini wameboresha zawadi za mchezaji bora wa mwezi wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za TFF, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura amesema kwa sasa mchezaji huyo bora atakuwa akipokea tuzo maalum, fedha taslim shilingi milioni moja pamoja na king’amuzi cha Azam TV.

Ofisa huyo wa TPLB amesema zawadi zilizoongezwa ni tuzo itakayokuwa ikitolewa na bodi hiyo pamoja na king’amuzi ambacho kitakuwa kikitolewa na wadhamini wa ligi hiyo upande wa matangazo ya runinga Azam TV, huku shilingi milioni moja iliyokuwepo tangu awali itaendelea kutolewa na wadhamini wakuu wa ligi ambao ni Vodacom Tanzania.

Wambura ameongeza kuwa tayari zawadi hizo mpya zilizotangazwa leo zimeanza kutolewa kwa aliyekuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba, Mudhathir Yahya kutoka Singida United na kesho (Januari 11, 2018) mchezaji bora wa mwezi Disemba 2017 anatarajia kutangazwa.