Habari za Kitaifa

OKWI ATOA TANGAZO LA KUBADILI JINA LAKE, SASA JINA LAKE ANALOTUMIA NI HILI HAPA…

 

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ameamua kubadili jina ambalo alikuwa analitumia kwenye mitandao ya kijamii.

Awali Okwi ambaye ni raia wa Uganda alikuwa akitumia jina la Emmo Sting akiwa anaunganisha maneno hayo kwa kuandika emmosting, lakini ameamua kubadili jina hilo.

Okwi amebadili jina hilo na sasa atakuwa akipatikana kwa jina lake halisi la Emmanuel Okwi ambapo jina hilo linaandikwa kwa kuunganishwa. Mara baada ya kuchukua maamuzi hayo, aliweka picha akiwa na jezi ya timu ya taifa ya Uganda na kuandika juu ya mabadiliko hayo.