Habari za Kitaifa

afc

KUELEKEA mchezo wa nusu fainali ya kombe la Sportpesa Super Cup, kocha mkuu wa Singida United Hemed Moroko amesema kuwa wapo vizuri kuikabili timu ya Gor Mahia.

 Akizungumza na Magic FM, Moroko amesema kuwa wamejipanga na wamefanyia mapungufu makosa waliyoyafanya katika mchezo wa kwanza hivyo mashabiki wao wategemee makubwa kuelekea mchezo huo.

 "Tunajua Gor Mahia ni timu yenye uzoefu mkubwa na wametuzidi sana hivyo tutajitahidi kuwakabili na kikubwa tutaingia na game plan mpya kabisa" alisema Moroko aliyechukua mikoba ya Hans Van Plujim.

 Singida United walitinga hatua hiyo baada ya kuwatoa AFC Leopards katika mchezo wa awali kwa njia ya mikwaju ya penati.