Habari za Kitaifa

Simba SC 1

 Hatua ya Nusu Fainali ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuendelea leo Alhamisi ambapo Simba itakutana na wababe wa Yanga, Kakamega HomeBoyz kwenye Uwanja wa Afraha. 

 Kakamega walifuzu kufika fainali baada ya kuifunga Yanga katika ufunguzi wa pazia la mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-1.

 Wakati Simba iliingia nusu kwa kuitoa ilitinga nusu fainali kwa changamoto ya penati 3-2 timu ya Kariobangi Sharks FC.

 Ikumbukwe kuwa jumla ya timu nne zimefuzu hatua hiyo ambazo ni Simba SC (Tanzania), Gor Mahia FC (Kenya), Singida United (Tanzania) na Kakamega HomeBoyz (Kenya).

 mosimba

WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC, wameandaa usiku wa tuzo kwa wachezaji, mashabiki na viongozi wa Simba kwa msimu uliomalizika wa 2017-18.

 Tuzo hizo zilizoandaliwa na mfanyabiashara maarufu na mdhamini wa Simba Mohamed Dewji zimepewa jina la Mo Simba awards zitakazotolewa usiku wa Juni 11,mwaka huu katika hoteli ya Regency hapa jijini Dar es Salaam.

 Tuzo hizo zinazotarajiwa kuwa za aina yake hapa nchini, zitaangalia vipengele kadhaa ndani ya kikosi hicho ikiwemo mchezaji bora, Kiungo bora, beki bora na mshambuliaji bora.

 Zingine ni tuzo ya shabiki bora wa msimu, Kiongozi bora pamoja na tuzo ya heshima ambayo mara nyingi hupewa wachezaji wa zamani waliofanya makubwa na klabu husika au mtu ywyote mwenye mchango mkubwa ndani ya klabu hiyo.

 

Simba itakuwa klabu ya kwanza kufanya tukio hilo hapa nchini na kwa uhalisia tuzo hizo zitatoa hamasa kwa wachezaji na hata baadhi ya klabu kuweza kuanzisha kitu kama hicho ili kuwapa hamasa wachezaji ikiwemo kiushindani.