Habari za Kitaifa

ditramnchimbi

MABINGWA wa Afrika Mashariki na kati Azam FC, wamefanikiwa kumsajili mshambuliaji Ditram Nchimbi aliyejuwa anakipiga kunako Njombe Mji.

 Nchimbi amesaini kandarasi ya miaka miwili kukitumikia kikosi hicho hivyo kuzitupa chini ofa za Simba, Yanga na Singida Unuted zilizokuwa zinamtaka kwa matumizi ya msimu ujao.

 Mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kupambana vilivyo, alikuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Njombe Mji licha ya kushuka daraja kutokana na kumaliza wa mwisho katika Ligi kuu Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni.

 Nchimbi anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Azam baada ya Donald Ngoma aliyetokea Yanga na Tafadwa Kutinyu aliyekuwa anakipiga na Singida United.

po

KONA YA MKEYENGE!

NA ABDULAH MKEYENGE 

NIMEWAHI kushuhudia Simba ikimfukuza kocha wake Moses Basena bila Basena kupoteza mchezo. Nikawahi kuwashuhudia mashabiki wa Simba wakitoka uwanjani kwa furaha timu yao ilipofungwa na TP Mazembe. Nimeyashuhudia matukio haya katika picha mbili tofauti.

Nyota wa mchezo wa kikapu Hasheem Thebeet ametembelea timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania inayojiandaa na michezo ya FIBA Zone V U18.

 Hasheem ambaye ni Mtanzania wa kwanza kucheza katika Ligi ya NBA ya Marekani, keshokutwa siku ya Jumapili, yaani Juni 10 atatumia muda wake mwingi kuwanoa vijana hao katika viwanja vya JMK Youth Park jijini Dar es Salaam.

 Uongozi ambao unasimamia vijana hao, umeomba wadau kujitokeze kwa wingi kuwaunga mkono vijana hao kwa kuwa bado wanahitaji michango ya hali na mali kufanikisha mashindano hayo, imeelezwa kuwa jumla ya mahitaji yanayohitaji ni Tsh milioni 100.