Habari za Kitaifa

NA JAPHARY LESSO

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania (Serengeti Boys), wametembeza dozi nzito kwa vijana wenzao wa Sudan baada ya kuwabugiza jumla ya mabao 6-0, katika mchezo uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Muyinga huko nchini Rwanda.

MCHEZO wa nusu fainali ya pili kombe la Shirikisho la Azam, unatarajia kupigwa kesho April 23, katika uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Mchezo huo utazikutanisha timu za Singida United watakaokuwa wakipepetuana na JKT Tanzani ya jijini Dar es Salaam.