Habari za Kimataifa

HUU MSHAHARA WA RONALDO NI KUFURU, JUVENTUS WAMEAMUA KUFANYA KWELI

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo atakuwa akipokea takriban pauni 73,000 kwa siku huku mkataba wake wa miaka minne ukiwa na thamani ya

pauni26m kwa mwaka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na mabingwa hao wa Itali kutoka Real madrid kwa dau la pauni99.2m. (Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Fabio Capello anasema kuwa hatua ya Ronald kujiunga na Juventus ni ya kijanja. Raia huyo wa Itali sasa anatarajia kwamba mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 30, ataelekea Chelsea. (Football Italia)

 Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, anapigiwa upatu na wachanganuzi wa soka kuchukua mahala pake Ronaldo katika klabu ya Real Madrid - na raia huyo wa Ubelgiji ataondoka Stamford Bridge iwapo Chelsea haitaonyesha ari ya kutaka kununua wachezaji wapya(Football London)

 Hatua hiyo ya Ronaldo itaiwezesha Juventus kuuza wachezaji ili kuafikia sheria za Fifa - na kiungo wa kati wa Itali Stefano Sturaro, 25, amevutia klabu za Newcastle na Wolves. (Birmingham Mail)

 Liverpool iko tayari kumununua mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 24, kwa dau la pauni80m . (TyC Sports, via Metro)

 Liverpool imeanzisha mazungumzo na Stoke kuhusu mkataba wa kumnunua kiungo wa kati wa Switzerland mwenye umri wa miaka 26 Xherdan Shaqiri, ambaye anaaminika kuwa na thamani ya pauni13m katika kandarasi yake . (Telegraph)

 Mkufunzi wa Napoli Carlo Ancelotti amemshirikisha beki wa Brazil na Chelsea David Luiz, 31, katika orodha ya wachezaji anaowalenga. (Mirror)

 Southampton itakamilisha makubaliano ya kibinafsi na beki wa Borussia Monchengladbach Jannik Vestergaard baada ya raia huyo wa Denmark , 25, kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu kwa uhamisho wa dau la pauni18m . (Sky Sports)