Habari za Kimataifa

BAADA YA KUSEPESHWA KOMBE LA DUNIA, KOCHA WA HISPANIA AAMUA KUACHIA NGAZI

Kocha wa Timu ya Taifa ya Hispania, Fernando Hierro (50) ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kuondoshwa katika michuano ya Fainali za Kombe la Dunia 2018, zinazoendelea nchini Urusi.

Hierro amefikia uamuzi huo ikiwa ni ikiwa hata mwezi mmoja haujatimia tangu Juni 13, 2018 alipoteuliwa kuwa kocha wa muda baada ya kocha wa taifa hilo Julen Lopetegui kufutwa kazi siku moja kabla ya kuanza michuano hiyo kufuatia kutangazwa kwake kuwa Kocha wa Klabu ya Real Madrid.

 Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Uhispania, Hierro ambaye ambaye aliwahi kuichezea Madrid amekataa kurejelea katika wadhifa wake wa wa zamani wa mkurugenzi wa michezo, badala yake ameamua kutafuta mambo mengine ya kufanya.